Kifungu cha 55
Article 55
Gavana hana wajibu wa kumjulisha Khalifah kuhusu kile alichotekeleza ndani ya mamlaka aliyopewa. Ikiwa tatizo jipya litajitokeza ambalo halina mfano uliotangulia, lazima kwanza amjulishe Khalifah kuhusu tatizo hilo, kisha aendelee kulingana na maagizo ya Khalifah. Ikiwa aliogopa kwamba tatizo lingezidi kuwa baya iwapo angechelewesha, anatekeleza hatua hiyo kisha ni lazima baadaye amjulishe Khalifah sababu ya kutomjulisha kabla.
The governor is not obliged to inform the Khalifah of what he has carried out within his authorised command. If a new problem arises which has no precedent, he has to inform the Khalifah about it first, and he then proceeds according to the instructions of the Khalifah. If he was afraid that the problem would be exacerbated if delayed, he carries out the action and then must inform the Khalifah later on about the reason for not informing him beforehand.
Ushahidi upo wazi kwamba Mtume (saw) aliwapa mamlaka magavana wake, na hakuwaagiza wamjulishe matendo yao yoyote, wala wao hawakuwa wakimripoti chochote. Badala yake, walikuwa wakitekeleza majukumu yao kwa uhuru kamili, kila mmoja akitawala katika uongozi wake kwa kutumia ijtihadi yake; hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Mu’adh, na ’Attab bin Asid, na Al-’Ala’ bin Al-Hadrami, na kwa magavana wote wa Mtume wa Allah ﷺ. Hili linaonyesha kwamba gavana hamjulishi Khalifah juu ya chochote katika matendo yake. Na katika jambo hili, yeye anatofautiana na msaidizi, kwani msaidizi lazima amjulishe Khalifah kuhusu kila kitendo anachokifanya, ilhali si wajibu kwa gavana kumjulisha Khalifah kuhusu lolote katika matendo yake.
The evidence is that the Prophet (phuh) empowered his governors and did not request them to inform him of what actions they undertook and they did not use to report to him about anything. Rather, they used to undertake their actions with full independence, each of them ruling in his leadership by his opinion; this was the manner of Mu’adh, and ’Attab Bin Asid, Al- ’Ala’ b. Al-Hadrami, and of all of the governors of the Messenger of Allah (pbuh) – which indicates that the governor does not inform the Khalifah about anything from his actions. And in this regard, he is different from the assistant, since the assistant must inform the Khalifah about every action that he undertakes, whereas it is not obligatory upon the governor to inform the Khalifah about any of his actions.
Ni wajibu kwa Khalifah kuchunguza kila kitendo cha msaidizi wake, ilhali si lazima kwake kuchunguza kila kitendo cha gavana, ingawa yeye huchunguza hali ya magavana na kufuatilia habari kutoka kwao. Kwa hiyo, gavana ana uhuru usio na mipaka katika utawala wake, ndiyo maana Mu'adh alipotumwa Yemen alimwambia Mtume ﷺ: "Nitatumia maoni yangu mwenyewe." Hii ni dalili kwamba gavana hamjulishi Khalifah, bali hutumia maoni yake. Si haramu kumwomba Khalifah shauri katika mambo muhimu, lakini hamuombi shauri katika mambo madogo ili maslahi ya watu yasicheleweshwe. Ikitokea jambo jipya, huliacha kwa maoni ya Khalifah, kwa sababu madaraka ya ugavana ni kwamba Khalifah humkabidhi gavana uongozi wa mji au eneo, ambao ni utawala juu ya watu wake wote, na udhibiti wa mambo yanayojulikana katika vitendo vyake. Hivyo basi, ikitokea jambo jipya ambalo halikujulikana hapo awali, huachwa kwa uchunguzi wa Khalifah, isipokuwa ikihofiwa kwamba kuchelewesha kutaleta madhara; katika hali hiyo gavana huchukua hatua juu ya jambo hilo kisha humjulisha Khalifah, kwa kuwa ni jambo ambalo halikuwahi kutokea kabla.
It is obligatory that the Khalifah scrutinise every action the assistant undertakes, whereas it is not necessary for him to scrutinise every action of the governor, though he studies the situation of the governors and scrutinises the news from them. Accordingly, the governor has unrestricted action in his governorship, which is why Mu’adh said to the Messenger (pbuh) when he was sent to Yemen “I will exert my own opinion.”; so this is evidence that the governor does not inform the Khalifah, rather he exercises his opinion. It is not forbidden to take the opinion of the Khalifah in the important issues, but he does not seek his opinion in unimportant issues in order that the interests of the people are not delayed. If something new occurs, he leaves it to the opinion of the Khalifah, because the empowerment of the governorship is that the Khalifah delegates the leadership of a city or region to the governor which is a governorship over all its people, and control in the known issues from his actions. So if a new issue which was not previously known occurred, it is left for the examination of the Khalifah, unless it was feared that this would be detrimental, in which case the governor undertakes the issue and then informs the Khalifah, since it was an issue that was unprecedented.