Kifungu cha 136
Article 136
Kila mtu anayemiliki ardhi analazimika kuitumia, na wale wanaohitaji msaada wa kifedha hupewa pesa kutoka Bayt Al-Mal ili waweze kuitumia ardhi yao. Ikiwa mtu yeyote atapuuza kuitumia ardhi kwa miaka mitatu mfululizo, huchukuliwa kutoka kwake na kupewa mtu mwingine.
Everyone that owns land is compelled to use it, and those that require financial help are given money from the Bayt Al-Mal to enable them to utilise their land. If anyone neglects utilising the land for three years continuously, it is taken from them and given to someone else.
Ushahidi wa hili ni kile Abu Yusuf alichopokea katika Al-Kharaj kutoka kwa Salim b. ‘Abd Allah (swt), kwamba Umar b. Al-Khattab (ra) alisema juu ya mimbari: “Atakayehuisha ardhi iliyokufa, basi ni yake, na yule aliyeizungushia uzio hana haki ndani yake baada ya miaka mitatu (ikiwa hakuilima).” Umar (ra) alisema haya mbele ya masahaba na wakisikia kikamilifu, wala hakuna miongoni mwao aliyemkemea, kwa hiyo ni ijmaa (makubaliano). Hii ni dalili wazi kwamba mtu akihuisha ardhi iliyokufa, au akaweka mawe au kitu chochote kinachoonyesha umiliki wake juu yake, basi anaimiliki. Hata hivyo, asipoitumia ardhi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, basi huchukuliwa kutoka kwake. Aliyeihuisha na aliyeizungushia uzio ni sawa kwa upande wa umiliki, na kwa upande wa kuondolewa kwao. Haiwezi kusemwa kwamba suala la umiliki limekomewa kwa mwenye kuhuisha: “atakayehuisha”, na kwamba suala la kuondolewa kwa umiliki, ikiwa ardhi ilipuuzwa, limekomewa kwa mwenye kuzungushia uzio na linamtenga mwenye kuhuisha, kwa maana kwamba umiliki ni kwa mhuishaji na kuchukuliwa ardhi ikiwa imepuuzwa ni kwa mwenye kuzungushia uzio pekee. Hii ni kwa sababu usemi huu ni wa mtindo wa kufuta kwa majazi (Hadhf), hivyo yule aliyezungushia uzio pia yumo chini ya umiliki, na mhuishaji yumo chini ya hukumu ya kuondolewa: kana kwamba Umar (ra) alisema: “atakayehuisha ardhi iliyokufa, basi ni yake, na hana haki juu yake baada ya miaka mitatu, na atakayezungushia uzio ardhi iliyokufa, basi ni yake na hana haki juu yake baada ya miaka mitatu.”