Ibara ya 105
Article 105
Watu wanaowakilisha maoni ya Waislamu kwa Khalifah ni Baraza la Ummah, na watu wanaowakilisha wananchi katika majimbo ni Mabaraza ya Majimbo. Inaruhusiwa kwa wasiokuwa Waislamu kuwa wanachama wa Baraza la Shura kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko yoyote dhidi ya dhulma yoyote inayofanywa na watawala au matumizi mabaya ya sheria za Kiislamu.
The individuals who represent the Muslims’ views to the Khalifah are the Ummah Council, and the individuals who represent the people in the provinces are the Provincial Councils. It is permitted for non-Muslims to be members in the Shura council for the sake of raising any complaints against any oppression by the rulers or misapplication of the laws of Islam.
Hili ni Baraza linaloundwa na watu wanaowakilisha maoni ya Waislamu kwa ujumla, ambalo Khalifah anaweza kulirejea ili kushauriana katika mambo mbalimbali. Nao ni wawakilishi wa Ummah katika kuwawajibisha watawala. Hili limetolewa kwa hoja kutokana na ushauriano wa Mtume wa Allah ﷺ na baadhi ya watu kutoka kwa Ansar na Muhajirina waliowakilisha watu wao. Pia linatokana na Mtume ﷺ kuwateua baadhi ya Maswahaba zake kwa ajili ya kushauriana (Shura). Alikuwa akiwarejea zaidi kuliko wengine ili kutafuta maoni yao, kama vile Abu Bakr (ra), Umar (ra), Hamza (ra), ‘Ali (ra), Salman Al-Farisi (ra), Hudhayfah (ra)….