Kifungu cha 106
Article 106
Wajumbe wa Mabaraza ya Mikoa wanachaguliwa moja kwa moja na wananchi katika mikoa yao, na idadi ya wajumbe wa Baraza lolote la Mkoa huamuliwa kwa kuzingatia uwiano wa wakazi wa mkoa huo kwa jumla ya watu wa Taifa.
The members of the Provincial Councils are directly elected by the people in their provinces, and the number of members of any Provincial Councils is decided according to the ratio of the inhabitants in such province to the whole population of the State.
Wajumbe wa Baraza la Ummah wanachaguliwa moja kwa moja na Mabaraza ya Mikoa. Mwanzo na mwisho wa vipindi vya Baraza la Ummah ni sawa na vile vya Mabaraza ya Mikoa. Wajumbe wa Baraza la Ummah wanachaguliwa, si kuteuliwa. Wao ni wawakilishi wa watu wa kutoa sauti za umma, na mwakilishi anapaswa kuchaguliwa na yule anayemwakilisha, wala asilazimishwe juu yake. Zaidi ya hayo, wajumbe wa Baraza la Ummah ni wawakilishi wa maoni ya watu, iwe ni watu binafsi au makundi; kwa hiyo kumjua mwakilishi wa watu katika eneo kubwa, na watu ambao hawajulikani sana, hakuwezekani isipokuwa mwakilishi huyu achaguliwe nao. Pia, Mtume wa Allah ﷺ hakuwachagua wale aliowashauri kwa msingi wa uwezo wao, umahiri wao na haiba zao; bali aliwachagua kwa sababu walikuwa viongozi miongoni mwa watu wao, bila kujali uwezo na umahiri wao. Katika Bay'a ya pili ya Al-'Aqabah, Waislamu waliompa Bay'a hawakuwa wanajulikana kwake, na ndiyo maana aliliacha suala la kuchagua viongozi kwao, kwa kusema: