Kifungu cha 139
Article 139
Serikali hairuhusiwi kuhamisha mali ya binafsi kuwa mali ya umma, kwa kuwa mali ya umma imethibitishwa na asili na sifa ya mali yenyewe, si kwa maoni ya Serikali.
The State is not permitted to transfer private property into public property, since public property is confirmed by the nature and characteristic of wealth and not by the opinion of the State.
Ushahidi ni maneno kutoka kwenye hadith iliyokubaliwa ya Mtume ﷺ kupitia Abu Bakra:
The evidence are the words from the agreed upon narration of the Messenger (pbuh) through Abu Bakra:
. إِنَّ دِمَاءكَُمْ وَأَمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ عَلَيْكُمْ حَ رَامٌ كَحُرْمَةِ يوَْمِكُمْ هَذَا فِي بلََدِكُمْ هَذَا « »... فِي شَهْرِكُمْ هَذَا .
. إِنَّ دِمَاءكَُمْ وَأَمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ عَلَيْكُمْ حَ رَامٌ كَحُرْمَةِ يوَْمِكُمْ هَذَا فِي بلََدِكُمْ هَذَا « »... فِي شَهْرِكُمْ هَذَا .
“Hakika! Damu zenu, mali zenu, na heshima zenu ni takatifu kwa kila mmoja wenu, kama utakatifu wa siku hii yenu, katika mji huu (Makka) wenu, katika mwezi huu wenu,” ambalo ni la jumla na linajumuisha kila mtu, hivyo ni haramu kuchukua mali ya mtu yeyote, awe Mwislamu au si Mwislamu, isipokuwa kwa sababu iliyowekwa na sheria. Kwa hiyo, ni haramu kwa Dola kuchukua mali ya mtu yeyote isipokuwa kwa sababu ya Shari’ah. Kwa msingi huo, ni haramu kwa Dola kuchukua mali ya mtu yeyote kuimiliki kwa kisingizio cha manufaa, au kuifanya mali ya umma kwa manufaa ya Ummah, kwa kuwa hadithi imekataza hilo, na manufaa hayafanyi kitendo hicho kiwe halali, kwa kuwa kuhalalishwa kwake kunahitaji ushahidi wa Shari’ah. Haiwezi kusemwa kwamba Imamu anaweza kufanya hivyo kama sehemu ya kusimamia maslahi ya Ummah, kwa kuwa yeye ana haki ya kusimamia mambo. Hii ni kwa sababu kusimamia mambo ni kushughulikia maslahi ya watu kulingana na kanuni za Shari’ah, wala si kushughulikia maslahi ya watu kulingana na maoni ya Khalifah. Kwa hiyo Khalifah hana mamlaka yoyote ya kuruhusu kile ambacho Allah (SWT) amekikataza, na akifanya hivyo, kitendo hicho kitachukuliwa kuwa dhuluma, ambayo atapelekwa mahakamani kwa ajili yake, na mali itarudishwa kwa mmiliki wake.