Ibara ya 107
Article 107
Kila raia aliye mtu mzima na mwenye akili timamu, ana haki ya kuwa mjumbe wa Baraza la Ummah au Baraza la Mkoa, awe mwanaume au mwanamke, Mwislamu au asiye Mwislamu; mjumbe asiye Mwislamu amezuiwa kutoa malalamiko kuhusu dhuluma za watawala au matumizi mabaya ya sheria za Kiislamu pekee.
Every citizen who is adult and sane, has the right to be a member of the Ummah Council or the Provincial Council, whether they are male, female, Muslim or non Muslim; the non-Muslim member is restriced to raising complaints regarding the oppression of the rulers or the misapplication of the laws of Islam.
Mtu yeyote wa Kiislamu mwenye uraia wa Dola, ikiwa amebaleghe na ana akili timamu, ana haki ya kuwa mwanachama wa Baraza la Ummah, bila kujali kama ni mwanamume au mwanamke. Hii ni kwa sababu Baraza la Ummah halina mamlaka ya kutawala, wala halihusiki na simulizi inayozuia mwanamke kuwa mtawala. Badala yake, lipo ndani ya suala la mashauriano (Shura) na uwajibikaji, ambalo ni haki ya wanaume na wanawake wote. Katika mwaka wa kumi na tatu wa Utume wa Mtume wa Allah ﷺ, yaani mwaka alipohamia Madina, walimwendea watu sabini na watano wa Kiislamu, miongoni mwao wakiwemo wanawake wawili, nao wote wakampa Bay'a ya pili ya Al-'Aqaba, ambayo ilikuwa Bay'a ya vita na mapigano na Bay'a ya kisiasa. Baada ya wote kumpa Bay'a, aliwaambia wote: