3. Shambulio la Waorientalisti
3. The Orientalist Attack
Hali ya Waislamu leo inatofautiana kabisa na historia yao tukufu ya zamani. Ni muhimu kwetu kuelewa jinsi na kwa nini hali kama hii imetokea. Kwa kweli, hili ndilo ufunguo wa kufufuka kwetu. Kwa hiyo, ni lazima kusoma kwa makini historia ya Uislamu, tangu wakati wa Dola ya Mtume ﷺ na kipindi cha ustaarabu na ushawishi wa Kiislamu uliofuata, mpaka leo, ili tuweze kutambua sababu kuu za udhaifu wetu.
The situation of Muslims today lies in stark contrast with their glorious past. It is important for us to understand how and why such a state of affairs has arisen. Indeed this is a key to our revival. To this end, it becomes necessary to study carefully the history of Islam, from the time of the Prophet’s (saw) State and the period of Islamic civilisation and influence that followed it, until today, in order that we may identify the main factors of our weakness.
Matokeo ya utafiti kama huu yanaonyesha kwamba kigezo kikuu ni kupungua kwa uwezo wa kiakili kwa hatua kwa hatua katika fikra za Waislamu kuhusu uelewa wao wa dini yao.
The result of such a study shows that the main factor is a gradual intellectual decline in the minds of the Muslims with regards to their understanding of their deen.