16 Maisha huko Madinah
16 Life in Madinah
Uislamu una mtindo maalum wa maisha unaotokana na mafundisho yake kuhusu maisha. Haya ndiyo msingi wa utamaduni wa Kiislamu, ambao unatofautiana kabisa na tamaduni nyingine zote. Unatambulika kwa mambo matatu:
Islam has a specific way of life derived from its concepts concerning life. These are the building blocks of the Islamic culture, which radically differs from all other cultures. It is characterized by three points:
Imejengwa juu ya 'Aqeedah ya Kiislamu;
1) It is founded on the Islamic ‘Aqeedah;.
2) Kigezo cha matendo katika maisha kinategemea amri na makatazo ya Allah, yaani maisha yanajengwa juu ya halali na haramu peke yake, na si jambo lingine lolote (kama vile manufaa au Maslaha);.
2) The criterion of actions in life is based on Allah’s commands and prohibitions, i.e. life is based on Halal and Haram and nothing else (such as benefit or Maslaha);.
3) Maana ya furaha ni kupata radhi za Allah, yaani amani ya kudumu ya moyo haiwezi kupatikana bila kwanza kupata radhi za Allah.
3) The meaning of happiness is to gain Allah’s pleasure, i.e. permanent peace of mind cannot be achieved without first gaining Allah’s pleasure.
Huo ndio mtindo wa maisha ya Kiislamu, aina ya maisha ambayo Waislamu huyatazama kwa heshima na kulenga kuyafikia. Ili jambo hilo litimie, ni lazima kuwepo na Dola inayotekeleza Uislamu kikamilifu na kutekeleza sheria zake bila ubaguzi. Waislamu walipohamia Madinah, waliishi maisha ya kipekee yaliyojengwa juu ya 'Aqidah ya Kiislamu. Aya za Qur'an zinazohusu kanuni za kijamii na za adhabu zilishushwa wakati huu, pamoja na aya zinazohusu mambo mengine ya ibada ambayo hayakuwa yameshushwa kabla. Zakat (sadaka ya lazima) na Swiyam (funga)ziliwekwa wajibu katika mwaka wa pili wa Hijrah. Adhana iliwekwa, na watu wa Madinah wakaisikia ikitolewa kwa sauti tamu ya Bilal bin Rabah mara tano kila siku. Miezi kumi na saba baada ya kuwasili kwa Mjumbe wa Allah ﷺ Madinah, Qiblah (upande wa kuswalia) kilihamishwa kuelekea Al-Ka'bah. Zilishushwa pia aya za Sheria ya Mwenyezi Mungu zinazohusu ibada, chakula, maadili, mahusiano na adhabu. Khamr (vileo) na nyama ya nguruwe vikakatazwa, na aya zinazohusu kanuni za adhabu na jinai zikashushwa, pamoja na zile zinazohusu miamala ya kibiashara, na katazo kamili la Riba katika aina zake zote, na kadhalika. Kila mara aya zilizohusu mambo ya maisha ya kila siku ya watu zilipomshukia Mjumbe wa Allah ﷺ, alizifafanua na aliwaamuru Waislamu kuzitii. Alisimamia mambo ya Waislamu kwa kutatua matatizo yao na kumaliza migogoro yao kwa kauli zake, vitendo vyake, na kwa kunyamaza kwake juu ya yale yaliyotokea mbele yake, kwani kauli yake ﷺ, vitendo vyake na kunyamaza kwake ni vyanzo vya Shari'ah, kama Allah (SWT) asemavyo katika Surat al-Najm,
That is the Islamic way of life, the kind of life Muslims look up to and aim to achieve. In order to make the above possible, it is essential to have a State that fully implements Islam and executes its rules without exception. When the Muslims migrated to Madinah, they led a distinguished way of life, with the Islamic ‘Aqeedah as its basis. The verses of the Qur’an concerning the social and penal codes came to be revealed at this time, in addition to the verses concerning other matters of worship which had not been revealed before. Zakat (alms) and Siyam (fasting) were decreed in the second year of the Hijrah. Adhaan was decreed and the people of Madinah listened to it being delivered in the sweet voice of Bilal ibn Rabah five times daily. Seventeen months after the arrival of Allah’s Messenger (pbuh) to Madinah, the Qiblah (direction of prayer) was transferred to the Ka’bah. The verses of Divine Legislation concerning matters of worship, diet, morals, relationships and penalties were revealed. Khamr (intoxicants) and the flesh of swine were forbidden, and the verses concerning the penal and criminal code were also revealed, as were those concerning business transactions, the complete forbidding of Riba in all its guises and so on. Every time the verses that spoke to the people’s affairs in everyday life were revealed to Allah’s Messenger (pbuh), he explained them and ordered the Muslims to abide by them. He (pbuh) looked after the Muslims’ affairs by solving their problems and settling their disputes by his sayings, actions and by his silence over what happened right in front of him, for his (pbuh) speech, actions and silence are all sources of the Shari’ah as Allah (swt) says in Surah al-Najm,
Wala hasemi kwa matamanio yake. Hiyo si chochote isipokuwa ufunuo unaofunuliwa. {An-Najm, 53:3-4}
“Nor does he speak of (his own) desire. It is only a Revelation that is revealed” [An-Najm, 53:3-4].
Maisha huko Madinah yaliendelea kufuata mwelekeo huo wenye mtazamo wake wa kipekee, yaani wa Kiislamu. Jamii ya Kiislamu, ambayo ni tofauti na jamii nyingine yoyote, ilikuwa hai na ikistawi wakati huo, ikijengwa juu ya dhana na hisia za Kiislamu. Sasa kanuni za Uislamu zilikuwa zikitekelezwa kikamilifu, zikitoa suluhisho na miongozo kwa Waislamu wote. Mjumbe wa Allah ﷺ alifurahi sana kuona kwamba Da'wah imefikia hatua hii, huku Waislamu wakiwa wametulia katika Dini yao, wakifuata kanuni zake kwa mtu mmoja mmoja na kwa pamoja bila kuogopa madhara wala mateso. Walitatua matatizo yao kwa mujibu wa kanuni za Allah, daima wakirejea kwa Mjumbe wa Allah ﷺ kuhusu mambo mapya yaliyojitokeza, wala hawakutoka nje ya mstari. Walitekeleza kanuni za Allah katika kila kitendo chao, na kwa njia hii walipata furaha na utulivu wa moyo. Waislamu wengi walimfuata Mjumbe wa Allah ﷺ kwa karibu ili wajifunze kutoka kwake, wahifadhi Qur'an na kupata elimu. Uislamu ulikua na kuenea, na Waislamu wakazidi kuimarika siku baada ya siku.
Life in Madinah continued to follow that course with its distinct viewpoint, i.e. the Islamic one. The Islamic society - which is different from any other - was alive and flourishing then, thriving on Islamic concepts and emotions and now that the rules of Islam were being comprehensively implemented, offering solutions and guidelines to all the Muslims. The Messenger of Allah (pbuh) was very pleased to see that the Da’wah had reached this stage with the Muslims settled in their Deen, abiding by its rules individually and collectively without fearing any harm or persecution. They solved their problems according to Allah’s rules, always referring new matters that had arisen to the Messenger of Allah (pbuh) and never stepping out of line. They applied Allah’s rules in every action and from this they achieved happiness and peace of mind. Many of the Muslims shadowed the Messenger of Allah (pbuh) in order to learn from him, to memorize the Qur’an and acquire knowledge. Islam grew and spread, and the Muslims became stronger day by day.