4.1 Mbinu Batili
4.1 The Invalid Methods
“Lakini hapana, (naapa) kwa Mola wako! Hawana Iymani mpaka wakufanye wewe (Ee Nabii) kuwa hakimu katika mizozo yao yote, kisha wasione kinyongo nafsini mwao kuhusu hukumu yako, na wanyenyekee kabisa kuikubali.” (TMQ al-Nisa’a, aya ya 65)
“But no, (I swear) by your Lord! They have no Iman until they make you (O Prophet) the judge in all their disputes and then they find no resentment in their souls regarding your judgement and they utterly submit to it” (TMQ al-Nisa’a, verse 65)
Mbinu Batili
The Invalid Methods
Kabla ya kujadili mbinu inayotokana na Ijtihad sahihi katika kufanya kazi ya kurejesha Khilafah, ni muhimu kuweka wazi mbinu potofu zilizopo leo, ambazo baadhi ya Waislamu wanazibeba. Mbinu hizo ambazo hazitokani na Ijtihad sahihi ni pamoja na mbinu ya taratibu (gradualism), na zile zinazotegemea dalili yenye kufanana na dalili ya kweli (Shubhat Daleel) ni pamoja na kupigana dhidi ya viongozi waliopo sasa. Kupitia haya, mtu ataona kwamba kuna haja ya dharura ya kuweka wazi mbinu sahihi.
Before the method based upon a correct Ijtihad in working to re-establish the Khilfah is discussed, it is important to highlight the false methods that exist today that are carried by some Muslims. Those methods that are not based upon a correct Ijtihad include gradualism, whilst those that are based upon a semblance of evidence (Shubhat Daleel) include fighting the present leaders. Through this, one will see that there is a pressing need to illustrate the correct method.